Mahakama kuu na idara kuu ya kuendesha mashtaka ya China zimewasilisha ripoti za kazi kwenye mkutano wa 4 wa Bunge la 12 la umma la China, ambazo zinatarajiwa kujadiliwa kesho kwenye mkutano huo.
Kwenye ripoti hizo, mahakama kuu na idara kuu ya kuendesha mashtaka zote zimesisitiza kuongeza nguvu katika kutekeleza sheria na kupambana na ufisadi.
Mwendesha mashtaka mkuu wa China Bw. Cao Jianming amesema, mwaka huu idara yake itaweka mkazo katika kutekeleza utaratibu wa kulinda usalama wa wanaotoa taarifa kuhusu uhalifu wa matumizi mabaya ya madaraka, kuendelea kuongeza nguvu katika kupambana na ufisadi wa maofisa wenye nyadhifa za juu, uhalifu wa kutumia vibaya madaraka unaotishia utekelezaji wa mikakati ya kiuchumi, mageuzi na kuharibu usalama wa mitaji ya taifa. Pia Bw. Cao amesisitiza ulazima wa kupambana na ufisada vijijini, na kuendelea kuwasaka maofisa wanaokutwa na makosa ya ufisadi ambao wamekimbilia nje ya nchi.
Naye mkuu wa mahakama kuu Bw. Zhou Qiang amesema, mwaka huu mahakama zitaimarisha kazi za kuhukumu kesi kubwa za uhalifu wa matumizi mabaya ya madaraka, na kupambana kithaibiti na ufisadi kwenye utekelezaji sheria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |