• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kuu ya China yawekeza miradi ya maji mkoani Tibet

    (GMT+08:00) 2016-03-13 19:18:56

    Katika miaka mitano iliyopita, serikali kuu ya China imewekeza yuan bilioni 22.3 ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 34 katika miradi ya maji katika mkoa unaojiendesha wa kabila la watibet. Uwekezaji huo umewanufaisha wakulima na wafugaji karibu milioni 1.8 mkoani humo, na kuhakikisha uzalishaji wa nafaka, usalama wa maji ya kunywa, utoaji umeme na masuala mengine ya maisha.

    Mkuu wa idara ya maji ya mkoa huo Bw. Dawa Tashi amesema, mwaka huu idara hiyo itajitahidi kukalimisha uwekezaji wenye thamani ya yuan bilioni 5 katika miradi ya maji, kuzindua mradi wa kuimarisha usalama wa maji kunywa vijijini, kuendelea kuhimiza ujenzi wa mradi wa usambazaji wa maji wa Lalo, na kuanzisha ujenzi wa mradi wa maji kwenye mto Xiang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako