• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Onyesho la utamaduni wa kichina lafanyika kwenye shule ya kimataifa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2016-03-30 20:52:58

    Jumanne wiki iliyopita, onyesho la utamaduni lililoandaliwa na darasa la Confucious mjini Nairobi lilifanyika kwenye shule ya kimataifa ya Braeburn, na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na wazazi zaidi ya mia moja.

    Onyesho hilo lilizinduliwa kwa maonesho ya vipaji vya wanafunzi, huku wanafunzi wa China na wa nchi za nje wa shule hiyo wakiimba kwa pamoja nyimbo maarufu za watoto za kichina. Baadaye, walimu na wazazi Wachina wakawaonesha na kuwafundisha watoto sanaa za maandishi ya kichina, kukata karatasi na michezo ya kutumia vijiti. Watoto walifurahi kushiriki kwenye mafunzo hayo kwa vitendo na kupata ufahamu zaidi kuhusu utamaduni wa China.

    Wazazi wa wanafunzi wa darasa la mafunzo ya lugha ya kichina walioshiriki kwenye onyesho hilo wote walisema, shughuli hiyo imewafahamisha zaidi wanafunzi wanaotoka nchi na tamaduni mbalimbali kuhusu mvuto maalumu wa utamaduni wa jadi wa kichina, na pia imeongeza hamu yao ya kujifunza lugha ya Kichina.

    Mkuu wa Darasa la Confucious mjini Nairobi Bw. Li Lin amesema, onyesho hilo la utamduni wa China linaweza kupanua upeo wa macho ya watoto kutoka nchi mbalimbali wanaosoma katika shule hiyo, na kuwasaidia wawasiliane na watu wenye tamaduni tofauti bila matatizo. Mbali na hayo, kushiriki kwenye shuguhli kama hizo pia kutawasadia kujifunza lugha ya kichina.

    Maneja mkuu wa shule ya kimataifa ya Braeburn Bw. Robert Williams amesema, baada ya maendeleo ya miaka miwili, darasa la lugha ya kichina kwenye shule hiyo limepiga hatua kubwa, na mafunzo ya lugha na shughuli za kiutamaduni vyote vimeendelea vizuri. Amesema, akiwa kiongozi wa shule hiyo, ataendelea kuunga mkono na kutoa msaada kwa miradi ya darasa la Confucious, na kuhimiza mafunzo ya lugha ya kichina yapanuliwe zaidi kwenye matawi ya shule hiyo.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako