• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikao cha maandalizi ya mkutano wa G20 chafanyika

    (GMT+08:00) 2016-04-05 20:25:16
    Kikao cha maandalizi ya mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa G20 kimefanyika mjini Nanjing, China, ambapo ajenda muhimu itakuwa uhimizaji wa maendeleo ya biashara na uwezekaji duniani.

    Mkutano wa wakuu wa G20 unatarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu mashariki mwa China, wakati biashara duniani inadidimia. Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya biashara kote duniani imepungua kwa silimia 12. Kutokana na muktadha huo, China, ikiwa mwenyeji wa mkutano huo, inajitahidi kuhimiza biashara na uwekezaji duniani kwa kushirikiana na nchi nyingine. Mkurugenzi wa idara ya biashara ya kimataifa chini ya wizara ya biashara ya China Zhang Shaogang amesema:

    "Ili kukabiliana na kudorora kwa biashara duniani, tunajadiliana na nchi nyingine za G20 kuhusu mkakati wa kuchochea ukuaji wa biashara, kwa kupitia kuimarisha usimamizi wa biashara, kupunguza gharama ya biashara, kuongeza ukusanyaji wa fedha, kukuza biashara ya kupitia mtandao wa Internet na kuongeza biashara ya huduma. Katika upande wa utungaji wa sera, tunajitahidi kuhimiza nchi za G20 kutoa mwongozo wa sera za uwekezaji duniani, ili kuongeza uratibu kati ya nchi mbalimbali".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako