• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jaribio la pili la ujasiriamali kwa kijana Qi Yang

    (GMT+08:00) 2016-04-08 08:17:04

    Mwaka jana kijana Qi Yang mwenye umri wa miaka 25 alirudi katika maskani yake Zhucheng mkoani Shandong kutoka Beijing, alikofanya kazi za vibarua kwa muda wa miaka 10, na kuanzisha mkahawa wake wa chakula cha nyumbani. Mkahawa wenye mapambo ya mtindo wa kale, chakula cha kifahari na mjasiriamali kijana aliyezaliwa baada ya miaka 90, yote hayo yamekuwa ni mambo ambayo wakazi wa huko wanapenda kuyazungumzia. Kila siku mkahawa wake unajaa wateja, na hali hii pia inamtia moyo Qi Yang.

    Miaka 10 iliyopita, kijana Qi Yang aliyehitimu kutoka shule ya Wushu alikuja mjini Beijing na kuanza maisha yake hapa Beijing. Kwa nyakati tofauti, alifanya kazi kama mtaalamu wa sanaa ya chai, mhudumu na mpishi. Mwaka 2010 Bw. Qi Yang ambaye alikuwa amefanya kazi katika sekta ya mikahawa kwa miaka karibu mitano, aliamua kujiingiza kwenye ujasiriamali kwa mara ya kwanza. Alianzisha kampuni ya biashara ya Sihairufeng ya Beijing, inayoshughulikia mambo kuhusu chakula na mikahawa. Lakini kutokana na uchambuzi usio wa sahihi kuhusu soko na fursa za biashara, Bw. Qi Yang alishindwa kuendelea. Hili lilikuwa pigo kubwa kwa Bw. Qi Yang, lakini pia lilimfanya afikirie upya mambo mengi. Bw. Qi anasema,

    "Naona sina woga wa kushindwa, lakini jambo baya zaidi ni pigo kubwa kwa imani yangu. Zamani niliona nina uwezo mkubwa wa kuchuma pesa na kufanya biashara, lakini niliposhindwa katika shughuli zangu niliona kweli ni vigumu sana kuendelea. Halafu nilianza kazi tena, ingawa mshahara ulikuwa mkubwa, lakini bado nilikuwa na wasiwasi moyoni, nikaona ni bora nianzishe tena shughuli. Kutokana na uzoefu wa kushindwa kwenye ujasiriamali kwa mara ya kwanza, nikaanza kufikiria kuwa si lazima kuanzisha shughuli zangu mjini Beijing. Kwa kuwa ni vigumu zaidi kujiajiri kutokana na kuwa kodi na gharama mbalimbali ikiwemo wafanyakazi ni kubwa sana, hivyo nikafikiria kurudi maskani yangu kujiajiri, kwani gharama zitakuwa ndogo zaidi."

    Ingawa jaribio la kwanza la kujiajiri kwa Bw. Qi Yang lilishindwa, lakini kutokana na upendo wake kwa sekta ya chakula na mikahawa na kupenda kuwa huru, alijitia moyo kujiajiri tena. Mwanzoni mwa mwaka jana, baada ya kupata mtaji kidogo Bw. Qi Yang aliamua kujiajiri tena.

    Baada ya kuchagua anuani kwa karibu nusu mwaka, Bw. Qi Yang alipanga nyumba iliyoko katika barabara ya Nanguan No. 100 mjini Zhucheng, na kuichukua kama jina la mkahawa wake. Baada ya kufanya ubunifu na marekebisho kwa miezi mitatu, mkahawa wa chakula cha nyumbani wa Bw. Qi Yang ulizinduliwa rasmi mwezi Septemba mwaka jana. Kila sehemu ya mgahawa huo ilikuwa inaonesha upekee wake. Katika mkahawa huo, kuna vyumba vitano maridadi vyenye majina mazuri ya Tangdi, Chayue, Qinggeng, Yudu na Luanju. Mianzi na maua ya peoni yamepandwa katika matuta yaliyoko katika kando mbili za mlango wa mkahawa huo, na wateja wanaweza kukaa mbele ya meza za chai zilizorekebishwa kutoka kinu cha mawe kupiga soga na kuonja chai. Bw. Qi Yang anasema,

    "Milango, madirisha, rafu na samani zote katika mkahawa wangu nilichagua mbao za mti wa elm wa sehemu ya kaskazini, ni katika hali ya kuwa na fedha za kutosha, vilevile matofali na kitalu cha maua mbele ya mlango vyote ni vitu vya kale. Muda ukiwa mrefu zaidi, vitu hivyo vikawa vinawavutia watu zaidi. Naamini baada ya miaka minne au mitano, mkahawa huo utawavutia watu zaidi. Baadaye baada ya siku kadhaa wakati hali ya hewa itakapokuwa joto zaidi, napanga kupanda Japanese creeper kando ya ukuta, na kupanda zabibu mwitu kwenye paa la nyumba, vilevile wisteria mbele ya mlango, nataka kuufanya mkahawa huo uwe maridadi wakati wa majira ya mchipuko, joto na mpukutiko, kwani vitoweo vyake viweze kuigwa na wengine, mpangilio wa mkahawa unaweza kuigwa pia, lakini maskini yako haiwezi kuigwa kwa urahisi. Nitafanya juhudi ili kuufanya mkahawa huo uwe wa kipekee mjini Zhucheng ndani ya miaka mitatu."

    Ukiwa mkahawa wa chakula cha nyumbani, bila shaka vitoweo vinapaswa kuwa na umaalum wake. Kila malighafi ya kitoweo, namna ya kukipikia na namna ya kukiweka kwenye sahani, hatua hizo zote zinasanifiwa na Bw. Qi Yang mwenyewe, na mpishi anafuata kigezo kilichowekwa kwa ajili ya kupika. Vitoweo katika mkahawa wa Bw. Qi Yang vinabadilika kwa kufuata majira, ili kuhakikisha vinaendana na mahitaji tofauti ya lishe katika kila majira. Baada ya kufanya hivyo kwa muda kadhaa, mkahawa huo unasifiwa na wateja wapya na waaminifu. Bw. Qi Yang anasema,

    "Hadi sasa, ni mimi mwenyewe ninayeamua kila kitoweo kinabuniwa, kwa mfano, marekebisho ya vitoweo, namna ya kupikia, kwa ladha gani, namna ya kukiwekea kwenye sahani. ninakagua kila hatua, na kubuni kitoweo, halafu nawaambia wapishi, wakapika kwa kufuata kigezo changu. Nyingine nitabadili vitoweo kwa kufuata majira, yaani kuzingatia mahitaji ya kiafya, na katika siku za kawaida, pia nitabadili baadhi ya vitoweo vidogo, kama nikiwa na malighafi nzuri au vitu maalum, nitavibadili kila wakati."

    Katika Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, marafiki na jamaa huwa wanajumuika, hivyo wakati huo ni fursa nzuri kwa mkahawa kuongeza mapato, lakini Bw. Qi Yang aliwapa wafanyakazi wake bonasi mapema na kuwafanya warudi maskani kusherehekea sikukuu. Bw. Qi Yang anasema,

    "Naona wafanyakazi ni muhimu zaidi kuliko wateja, kwa sababu wafanyakazi wakiwa na furaha, wateja wakaweza kuhudumiwa vizuri na kuwa na furaha. Shughuli za mkahawa na chakula zinaonekana kuwa na furaha nyingi, lakini kwa kweli ni kazi ngumu. Mapumziko ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ya China ni wiki moja tu, tunaweza kuchuma pesa gani? Kwa nini nisiruhusu wafanyakazi kurudi maskani kusherehekea sikukuu hiyo? Mwaka unaofuata bado tunatakiwa kufanya bidii kwa mwaka mzima. Mara kwa mara tunakaa pamoja kupiga soga matumaini yetu na mpango wetu, kwa kweli jambo linalonigusa ni kwamba, matumaini yao ni kuwa pamoja nami kutimiza lengo langu mwaka kesho."

    Hivi sasa Bw. Qi Yang amepevuka zaidi. Baada ya jaribio lake la kwanza la ujasiriamali kushindwa, sasa yuko makini zaidi kuhusu mpango wake wa siku za usoni. Bw. Qi Yang anasema,

    "Ninatunga mpango wa mwaka kesho tu, kila mwaka natunga vizuri mpango wa mwaka mmoja, baada ya kumalizika kwa mwaka huu natunga mpango wa mwaka kesho, ni lazima nifuate hali halisi. Mpango ninaoutunga ni lazima nikamilishe mwaka kesho, tena uwe unatekelezeka. Ujasiriamali unahitaji hali hiyo, ama sivyo tukizungumzia matumaini tu, haina maana, la muhimu ni kufuata hali halisi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako