• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtunzi wa hadithi za watoto wa China ashinda tuzo ya Hans Christian Andersen

    (GMT+08:00) 2016-04-12 06:35:33

    Mtunzi wa hadithi za watoto wa China ambaye pia ni profesa wa Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Cao Wenxuan ameshinda tuzo ya Hans Christian Andersen kwa mwaka huu katika maonesho ya 53 ya Vitabu vya Watoto ya Bologna yaliyofanyika nchini Italia. Cao ni mtunzi wa kwanza kutoka China aliyeshinda tuzo hiyo ambayo ni ya ngazi ya juu zaidi kimataifa inayotolewa kwa mtunzi na mchoraji wa picha kwa ajili ya vitabu vya watoto. Huu ni wakati mwingine wa kuona fahari kwa sekta ya fasihi ya China baada ya mtunzi mwingine aitwaye Mo Yan kushinda tuzo la Noble mwaka 2012.

    "Ifuatayo ni tuzo ya mtunzi, anayeshinda tuzo hiyo ni Cao Wenxuan."

    Tuzo ya Hans Christian Andersen kwa mwaka 2016 ilitolewa usiku wa Jumatatu iliyopita kwenye Maonesho ya Vitabu vya Watoto ya Bologna, wakati jina la Bw. Cao lilipotangazwa na mwenyekiti wa tume ya wachaguzi wa tuzo hiyo Bibi Patricia Aldana, watu waliohudhuria hafla hiyo walishangilia kwa kupiga makofi.

    Tuzo hiyo ya kimataifa ilianzishwa mwaka 1956 na Muungano wa kimataifa wa vitabu vya watoto IBBY, ambayo inatolewa kila baada ya mwaka mmoja, ikiwemo tuzo ya mtunzi na tuzo ya picha. Lengo la tuzo hiyo ni kuwasifu na kuwashuruku wale wanaotoa michango inayodumu kwa shughuli za fasihi ya watoto. Ikiwa ni heshima kubwa zaidi kwa watunzi wa vitabu vya watoto duniani, watu wameipa tuzo ya Hans Christian Andersen jina la "tuzo ndogo ya Noble".

    Katika orodha ya wagombea wa tuzo hiyo kwa mwaka huu, watunzi wote watano waliopendekezwa ni hodari katika sekta ya fasihi duniani. Sababu zilizomfanya Cao kuchaguliwa na waandaaji wa tuzo hiyo, sio tu ni uzuri wa fasihi ulioonyeshwa kwenye vitabu alivyoviandaa, muhimu zaidi ni kwamba, maisha ya utotoni aliyoeleza yana umaalumu wa kipekee wa kichina, ambao watoto wa nchi nyingine duniani hawana mazoezi nao.

    "Nadhani labda fasihi yangu inalingana zaidi kigezo cha uchaguzi wa tuzo ya Hans Christian Andersen. Kwani kigezo hicho kinazingatia zaidi ufasihi na sanaa, ambavyo ni muhimu zaidi. Naona fasihi yangu kweli inalingana sana na kigezo hicho. Tangu nilipoamua kushughulikia fasihi ya watoto, ama niseme fasihi, nimeendelea na msimamo huo huo juu ya fasihi. Ukiandaa fasihi moja, ni lazima kuiandaa vizuri kama unavyoandaa sanaa moja. Sababu nyingine ni kuwa nilitumia sana rasilimali iliyopo nchini kwangu kuhusu kuandaa fasihi. Hadithi hizo moja baada ya nyingine haziwezi kutokea katika sehemu yoyote duniani, zitatokea tu hapa China. Lakini kauli mbiu za hadithi hizo zinahusiana na binadamu wote, ni mada ya pamoja kwa binadamu."

    Mtunzi mmoja anaruhusiwa kushinda tuzo ya kimataifa ya Hans Christian Andersen mara moja tu katika maisha yake. Hapo awali watunzi kadhaa wa vitabu na picha katika vitabu kutoka China waliwahi kuorodheshwa kugombea tuzo hiyo, lakini walishindwa. Kutokana na ushindi wa Cao, nguvu ya fasihi ya China imeonesha uhai wake mkubwa. Akitoa tathmini wakati wa kutangaza mshindi wa tuzo ya Hans Christian Andersen, mwenyekiti wa tume ya wachaguzi Bibi Patricia Aldana alisema, fasihi ya Cao Wenxuan inaeleza maisha ya mtoto mhusika mkuu mwenye furaha na taabu anapokabiliwa na changamoto mbalimbali.

    "Ushindi wa Bw. Cao Wenxuan umekubaliwa kwa kauli moja na waandaaji wote wa kamati. Fasihi yake ni nzuri sana, na imekuwa ni mfano mzuri wa kuigwa kuhusu watoto kukabiliana na maisha yenye taabu na changamoto, na fahisi yake inapendwa na wasomaji watoto wengi sana."

    Cao anaheshimu fasihi na sanaa, tangu aanze kushughulikia kazi ya utunzi, alikuwa anaandaa fasihi zenye umaalum wake kwa kushikilia kufuata kanuni maalum za uandishi. Anaweka wazi kuwa yeye sio mtunzi wa vitabu vya watoto tu, vitabu anavyoandika vinawafanya watu wazima kuangalia dunia hii kupitia macho safi.

    "Hii inaelezwa katikati ya mistari katika fasihi hii. Napendelea mtazamo halisi wa dunia, wala sio mtazamo wa dunia wenye utatanishi, fasihi ya watoto ndiyo inayoweza kukidhi matarajio yangu hayo. Nataka kuongeza furaha yenye maana kwa dunia hii mbele yangu, fasihi ndiyo inachangia matakwa hayo."

    Takriban watu wote wanaona fasihi ya watoto ni fasihi inayowafurahisha watoto. Lakini Bw. Cao Wenxuan hakukubali maoni hayo. Anasema furaha siyo sifa bora zaidi ya mtu mmoja. Ndiyo maana watunzi hueleza hadithi zenye masikitiko ambazo kweli zinatokea katika maisha ya kila siku. Vitabu vyake ni kama fumbo, ambavyo inakamilisha zaidi utaratibu mzima wa fasihi ya watoto nchini China.

    "Vitabu vyangu huenda vitaboresha zaidi utaratibu wa fasihi ya watoto ya China, simaanishi tusitunze vitabu vinavyowafurahisha watu, bali watoto hawafai kusoma vitabu kama hivyo tu, mbali na hayo wangetakiwa kusoma "Nyumba zinazojengwa na majani", Alizeti za shaba", "Ding ding dang dang" na nyinginezo, huu ndio ufanisi ama matokeo ambayo nataka kuona."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako