• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya biashara ya China yasema biashara ya nje inaendelea kwa utulivu

  (GMT+08:00) 2016-04-07 20:11:50

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Shen Danyang amesema, biashara ya nje ya China inaendelewa kwa utulivu, ingawa inakabiliwa na shinikizo kubwa.

  Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wizara hiyo, mabadiliko ya kiwango cha sarafu ya China RMB, kuongezeka kwa gharama, kupungua kwa mahitaji kutoka nje, na ugumu wa ukusanyaji wa fedha zimekuwa changamoto kuu zinazoikabili bishara ya nje ya China. Uchunguzi huo pia umegundua kuwa, mamlaka za biashara za nchi za kikanda zina imani na utendaji wa China katika biashara ya kimataifa, na zinaona kuwa China itadumisha na hata kuongeza mgao wake katika soko la kimataifa.

  Habari nyingine zinasema, thamani ya biashara kati ya China na nchi husika za "Eneo la Kiuchumi la Njia Hariri na Njia Hariri ya Baharini ya Karne 21" kwa mwaka jana ilifikia dola bilioni 995 za kimarekani, ambayo imechukua robo ya thamani ya jumla ya biashara ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako