Taarifa iliyotolewa Ijumaa na mawaziri wa fedha na wakuu wa benki za nchi za G20 inasema, uchumi wa dunia bado unakabiliwa na shinikizo ya kupungua na hali isiyojulikana.
Jumanne wiki iliyopita, Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limeshusha makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu hadi asilimia 3.2, likisema uchumi wa dunia unakua kwa kasi ndogo, hali ambayo inafanya uchumi huo ukabiliwe na hatari.
Taarifa ya G20 aidha inasema migogoro, ugaidi, mawimbi ya wakimbizi na uwezekano wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya zinaleta utatanishi kwa mazingira ya kiuchumi ya dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |