Mfugaji wa kabila la wamaasai kutoka Tanzania ameshinda tuzo ya mazingira ya Goldman kwa mwaka huu, kutokana na njia yake ya kipekee ya kulinda mazingira na jamii yake kwa ujumla.
Tuzo hii inatolewa kila mwaka katika mabara yote kwa watu hodari kwenye uhifadhi wa mazingira, ili kuwatambua wanaharakati jasiri kwa mchango wao katika kuhifadhi mazingira na jamii zao. Mwaka huu tuzo hiyo kwa bara la Afrika imeenda kwa Bw Edward Loure.
Bw Loure ameshinda tuzo hiyo kutokana na juhudi zake katika kuhakikisha ekari laki mbili za ardhi katika eneo la jamii yake zinapatiwa haki miliki ya jamii yake, na si watu binafsi.
Tuzo ya mazingira ya Goldman ilianzishwa mwaka 1989 na viongozi wa kiraia wa San Fransisco, na washindi wanachaguliwa na jopo la majaji wa kimataifa kutokana na majina yanayopendekezwa na mtandao wa kimataifa na watu binafsi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |