Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mtwara mwishoni mwa wiki iliyopita, Juma alisema ugonjwa huo unaweza kukausha mikorosho kwa muda mfupi.
Aliwataka wakulima kutoa taarifa za kuingia kwa ugonjwa huo kwenye maeneo yao ili waweze kupatiwa elimu jinsi ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Juma alisema licha ya kuwapo kwa wataalamu wa kutosha nchini wa kuweza kuyabaini magonjwa na kuyafanyia utafiti, bodi hiyo imefanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti Naliendele ili kuona watakavyosaidia wadau wa zao hilo kupambana na kuondoa ugonjwa huo.
Mtafiti kiongozi wa korosho ambaye pia ni mtaalamu elekezi wa zao hilo barani Afrika wa kituo hicho, Profesa Peter Masawe alisema ugonjwa huo umekuwa ukiathiri mikorosho ya zamani na unasambaa kwa kasi zaidi.
Profesa Masawe alisema baada ya kuibuka kwa ugonjwa huo nchini kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walifanya utafiti na kubaini kuwa ni fangasi.
Aliiomba Serikali kuwekeza fedha katika tafiti kutokana na kutumia fedha nyingi.
Mtafiti mstaafu wa kituo hicho, Dk Shomari Shamte alisema ugonjwa huo unasababishwa na vimelea aina ya uyoga ambavyo vinajulikana kama Fusarium oxysporum.
Alisema hali hiyo husababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yanayochangia vimelea hivyo kushambulia mikorosho kutokana na kuwa na uwezo wa kuishi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |