• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza nguvu katika uhifadhi wa mabaki ya kale

    (GMT+08:00) 2016-04-20 21:08:51

    Mkutano wa kazi ya kuhifadhi vitu vya kale nchini China ulifanyika Jumanne wiki iliyopita hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China alitoa maagizo ya kuongeza nguvu kwenye uhifadhi wa vitu vya kale, kuhimiza matumizi ya vitu hivyo kwa njia mwafaka, na kujitahidi kutafuta njia ya uhifadhi na matumizi ya vitu vya kale inayolingana na hali halisi ya China.

    Hivi karibuni documentary moja ya China iitwayo "Natengeneza vitu vya kale kwenye kasri la wafalme" imetazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa Internet. Documentary hiyo si kama tu imefahamisha kwa jamii kazi ya watengenezaji wa vitu vya kale wasiofuatiliwa sana, bali pia imeinua mwamko wa umma kuhusu uhifadhi wa vitu vya kale.

    Ukweli ni kwamba, mambo yanayooneshwa kwenye documentary hiyo ni mifano kadhaa tu ya kazi ya wahifadhi wa vitu vya kale. Mkurugenzi wa idara ya kitaifa ya vitu vya kale ya China Liu Yuzhu amesema, katika mpango wa 12 wa maendeleo ya miaka mitano, China imeongeza nguvu kidhahiri kwenye uhifadhi wa vitu vya kale, na kazi mbalimbali zimeendelea kwa utaratibu.

    "Katika mpango wa 12 wa maendeleo ya miaka mitano, mafanikio yaliyopatikana kwenye kazi ya kuhifadhi vitu vya kale nchini China ni pamoja na kuinuka kidhahiri kwa mwamko wa umma; kazi za kuokoa na kuhifadhi mabaki ya kale kwenye miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa lambo la magenge matatu na mradi wa kusafirisha maji kutoka kusini hadi kaskazini, miradi ambayo imemalizika bila matatizo; Tatu ni kufanikiwa kwa mara 13 mfululizo kuorodhesha mabaki mbalimbali ya kale kwenye urithi wa kiutamaduni duniani, na kuifanya idadi ya mali za urithi wa kiutamduni duniani nchini China ichukue nafasi ya pili duniani."

    Mbali na hayo, miradi muhimu ya uhifadhi wa sanamu ya budhaa ya Avalokitesvara kwenye wilaya ya Dazu mjini Chongqing, na kasri la kifalme la majira ya joto pamoja hekalu zilizoko karibu mjini Chengde mkoani Hebei imekamilika, mradi mkubwa wa kuhifadhi ukuta mkuu umemalizika kama ilivyopangwa, na miradi mingine ya uhifadhi wa mabaki ya kale kwenye sehemu mbalimbali nchini China pia imemalizika kwa utaratibu.

    Kwenye msingi wa kuokoa na kuhifadhi mabaki ya kale, katika miaka ya hivi karibuni, matumizi mwafaka ya vitu vya kale pia yametoa mchango muhimu kwenye kuhimiza maendeleo na kuboresha maisha ya watu. Kutumika tena kwa baadhi ya mabaki ya viwanda vya zamani yakiwemo majengo ya asili ya kiwanda cha bia cha Qingdao, kumekuwa mapambo ya kihistoria na ya kiutamaduni katika miji; Bustani za kitaifa za mabaki ya kale ikiwemo kasri la wafalme la enzi ya Tang lililoko mjini Xi'an mkoani Shannxi, zimeonesha manufaa ya kijamii na kuhimiza maendeleo yenye uwiano ya uchumi na jamii. Aidha, katika miaka ya hivi karibuni, majumba ya makumbusho ya ngazi mbalimbali yamefanya maonesho kadhaa ya mabaki ya kale, ambayo yamefuatiliwa sana kwenye jamii na kusaidia kuongeza ufahamu wa umma kuhusu uhifadhi wa mabaki ya kale. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa nchini China kwa ujumla kuna majumba ya makumbusho 4,510, na 3,717 kati yao yanahudumia umma bila malipo.

    Waziri wa utamaduni wa China Luo Shugang amesema, katika mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano, China itajitahidi kupanua njia za matumizi ya mabaki ya kale, zikiwa sambamba na uhifadhi wa mabaki hayo, ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya kiutamaduni kwenye jamii.

    "Tunapaswa kuonesha kadri iwezekanavyo uwezo kutoa huduma za kiutamaduni kwenye jamii na kuelimisha umma kwa kutumia mabaki ya kale, pia tunapaswa kuendelea kuongeza idadi ya majumba ya makumbusho yanayotoa huduma bila malipo, kuongeza nguvu katika kuinua kiwango cha maonesho kwenye majumba yetu, na kuhimiza idara za uhifadhi wa vitu vya kale kufunguliwa kwa umma bila malipo kadri inavyowezekana."

    Hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China alipotoa maagizo kuhusu kazi ya kuhifadhi vitu vya kale, alizitaka idara husika ziongeze nguvu zaidi kwenye kazi hiyo, na kuhimiza matumizi mwafaka ya vitu vya kale, ili viweze kuwanufaisha zaidi wananchi. Rais Xi pia amezitaka idara za kuhifadhi vitu vya kale kwenye ngazi mbalimbali zijitahidi kushirikisha nguvu za kijamii na kutafuta njia ya kuvihifadhi na pia kuvitumia vitu vya kale inayolingana na hali halisi ya China.

    Naye waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa, idara husika zinapaswa kuweka mpango unaojumuisha uhifadhi na matumizi mwafaka ya mabaki ya kale, kuonesha thamani za kihistoria, kiutamaduni na kisayansi ya mabaki ya kale kwenye msingi wa uhifadhi madhubuti, na kuendeleza uwezo wa vitu vya kale katika kutoa huduma za kiutamaduni na kuelimisha umma. Bw. Li Keqiang pia amezitaka idara husika zihamasishe nguvu za pande mbalimbali, ili kushirikisha jamii nzima kwenye kazi ya uhifadhi wa mabaki ya kale.

    Maelekezo kuhusu kuimarisha zaidi kazi ya kuhifadhi vitu vya kale yaliyotolewa hivi karibuni na Baraza la serikali la China pia yametaka jamii ishirikishwe kwenye uhifadhi wa mabaki ya kale, na kwa baadhi ya majengo ya kale yanayomilikiwa na watu binafsi, mfuko wa uhifadhi wa vitu vya kale unapaswa kuanzishwa ili kukusanya fedha kwa ajili ya kuyahifadhi. Mkurugenzi wa bodi ya Mfuko wa uhifadhi wa vitu vya kale ya China Li Xiaojie amesema, mwaka huu mfuko huo utafanya majaribio kwenye wilaya ya Songyang mkoani Zhejiang na kutoa ufadhili kwa kazi za ukarabati na uhifadhi wa majengo ya kale yanayomilikiwa na watu binafsi.

    "Mwaka huu mfuko wetu utaanzisha harakati ya kuokoa majengo ya kale yanayomilikiwa na watu binafsi kwenye vijiji vyenye historia ndefu, ambapo wamiliki watakusanya nusu ya fedha zinazohitajika, na mfuko wetu utatoa nusu nyingine. Wakati huohuo, mfuko wetu pia utashirikisha vyuo vikuu na taasisi za usanifu kwenye kazi ya ukarabati wa majengo hayo, na pia tutahamasisha makampuni yawekeze au kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na kuhifadhi mazingira kwenye vijiji hivyo. Lengo letu ni kupata uzoefu, na kujitahidi kutafuta ufumbuzi wa kuhifadhi na kutumia majengo ya kale yanayochukua zaidi ya asilimia 60 ya majengo yote kwenye vijiji kama hivyo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako