• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa amani Afrika ni muhimu kwa maendeleo

    (GMT+08:00) 2016-04-22 06:55:40

    Uchaguzi wa amani barani Afrika, bara ambalo siku za nyuma lilikumbwa na vurugu zinazohusiana na uchaguzi, umeanza kushuhudiwa na hivyo kuhakikisha kuendelea kuwa na msingi imara wa utulivu na maendeleo.

    Mwaka huu pekee, zaidi ya nchi 10 za Afrika zimefanya uchaguzi, na karibu nchi zote zimehitimisha zoezi hilo kwa amani. Nchi hizo ni pamoja na Chad, Benin, Niger, Uganda, Jamhuri ya Kongo, Djibouti na Visiwa vya Comoro.

    Hadi mwaka wa 2,000 baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vikilitaja bara la Afrika, kama lisilo na matumaini. Lakini sasa bara hilo lenye idadi kubwa ya nchi zinazoendelea duniani, limeshuhudia ukuaji wake mkubwa wa kiuchumi, utulivu wa kisiasa, na vyombo vya habari vimebadili vichwa vya habari na kuwa "Afrika inaibuka."

    Licha ya kuwa na chaguzi zenye mizozo siku za nyuma, chaguzi za hivi karibuni zimekuwa za amani. Kukubali matokeo kwa washindi pamoja na walioshindwa ni ishara ya kukomaa kwa demokrasia.

    Kwa nchi zinazoanza kukuza uchumi wake, kudumisha kasi ya ukuaji wa uchumi ni msingi wa uchaguzi wa amani kwani amani inapunguza hali ya kutokuwa na uhakika na hatari, na kuchangia ukuaji wa uchumi.

    Takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia zinaonyesha kwamba ukuaji wa uchumi wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ulikuwa asilimia 6.8 kati ya mwaka wa 2003-2008.

    Pili, hatua ya viongozi wengi kukubali kuondoka madarakani baada ya muda wao uliopangwa kikatiba kumalizika pia imechangia utulivu na maendeleo barani Afrika.

    Muhammadu Buhari, mgombea wa upinzani wa chama cha All Progressives Congress nchini Nigeria, alitangazwa rais baada ya kumshinda Rais Goodluck Jonathan katika uchaguzi wa rais wa Nigeria mwaka 2015. Kwa mara ya kwanza nchini humo, mpinzani alimshinda kiongozi aliye madarakani.

    Tatu, kuongezeka kwa ufuatiliaji wa uchaguzi na kutoa taarifa kunakofanywa na Umoja wa Afrika, taasisi za kikanda kama vile vikundi vya kiraia, pia vimekuwa na umuhimu mkubwa kwa uchaguzi wa amani.

    Wito uliotolewa hivi karibuni wa Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma wa kupiga kura kwa amani na uwazi barani Afrika unafaa kutiliwa maanani kwani utalinda utulivu na maendeleo.

    Afrika inaweza kusonga mbele na kupata maendeleo ikiwa, kama kutatokea migogoro, wagombea na wafuasi watasuluhisha kwa njia ya mazungumzo na taratibu za kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako