KRA yawataka wamiliki wa nyumba za kupanga kulipa kodi
(GMT+08:00) 2016-04-22 19:34:18
Mamlaka ya forodha ya Kenya imewalaumu wamiliki wa nyumba za kupanga dhidi ya kile wanachosema ukwepaji wa ulipaji kodi. Kauli hiyo inakuja miezi tisa tu baada ya kipindi cha msamaha kilichotolewa na mamlaka ya kodi ya Kenya kwa wamiliki wa nyumba za kupanga kutarajiwa kumalizika juni mwaka huu. Hata hivyo mamlaka hiyo imesema ni wamiliki wa nyumba za kupanga 1,000 pekee ambao wameitikia wito wa kulipa kodi ndani ya kipindi hicho cha msahamaha. Hivi sasa mamlaka hiyo imesema inawafuatilia wamiliki wa nyumba za kupanga elfu 20 kote nchini Kenya ili kuinua mapato ya kodi hadi bilioni 3 kutoka kwa sekta hiyo. Mamlaka hiyo imesema kampeini hiyo inalenga kuhamasisha wakenya umuhimu wa wamiliki wa nyumba za kupanga kulipa kodi kwa wakati.