• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania ndio mmiliki wa kampuni ya General Tyres Arusha

    (GMT+08:00) 2016-04-22 19:35:59
    Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wa Tanzania Bw Charles Mwijage amesema hivi sasa kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre Arusha kinamilikiwa na serikali baada ya serikali kununua asimilia 26 kutoka kwa mbia wake. Akizungumza bungeni, Bw Mwijage amesema serikali imeweka dhamana ya kusimamia na kuendesha kiwanda hicho, chini ya shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kwamba tangazo la Serikali (GN) kuhusu uamuzi huo litatolewa wakati wowote kuanzia sasa. Amesema dhamira ya serikali ni kuona kiwanda hicho kinaanza kuzalisha matairi mapema iwezekanavyo. Pia shirika hilo litatoa majibu ya kiufundi na kijamii na kwamba ni lazima lizingatie maoni ya wadau wa sekta husika kwa ajili ya kuboresha kiwanda hicho. Aidha, mradi huo utaendeshwa chini ya menejimenti ya rasilimali watu wenye weledi katika biashara ya matairi na bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini. Awali kiwanda hicho kiliacha uzalishaji mwaka 2009 baada ya serikali kukosa fedha za kukiendesha huku mbia mwenza kampuni ya Continental AG, kutokuwa tayari kuendelea na uwekezaji huo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako