Akizungumza na radio China kimataifa, mwenyekiti wa kamati hiyo Hawa Ghasia amesema ukuaji wa sekta ya viwanda katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango huo ulikuwa asilimia 6.6 chini ya lengo la kufikia wastani wa asilimia 11 mwaka 2015.
Amesema jambo hilo haliridhishi maendeleo ya uchumi wa viwanda na kusisitiza kuwa sekta ya madini katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya kwanza haukuwa na mabadiliko makubwa kwenye Pato la Taifa kwa mwaka 2010. Kwa upande wake, naibu msemaji wa upinzani bungeni wa wizara ya fedha na Mipango Bw David Silinde amelitaka bunge kupitisha azimio ili kamati ya bunge kuhusu bajeti iwasilishe muswada wa sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |