Akizungumza bungeni, naibu waziri ofisi ya rais, Bw Antony Mavunde amesema utaratibu wa kugawa fedha hizo unaandaliwa na baraza la uwezeshaji wananchi kwa kushirikiana na wizara ya Utawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.Ameongeza kuwa vigezo ambavyo vimekuwa vikitumika katika kutoa mikopo na mitaji kwa vijana ni umri usiozidi miaka 35 ambapo vijana watahitajika kujiunga na Saccos za wilaya na kuunda vikundi na kuvisajili kisheria.Amesema ili kuhakikisha vijana wanakuwa wajasiriamali na wanaweza kupatiwa mikopo na mitaji, serikali imejiwekea mikakati ya kutambua vijana na mahitji yao katika ngazi mbalimbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali ya vijana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |