• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bomba la mafuta la Uganda litapitia Tanzania

    (GMT+08:00) 2016-04-25 09:17:46

    Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wametangaza kuwa bomba la mafuta la Uganda kutoka Hoima hadi Bandari ya Tanga litapitia Tanzania, mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za kimarekani bilioni 4.

    Viongozi hao wamefanya uamuzi huo kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika mjini Kampala, ambao pia umeamua kuwa bomba jingine la mafuta litajengwa nchini Kenya kutoka eneo la Lokichar hadi bandari ya Lamu.

    Vyombo vya habari vya Uganda vimeona kuwa, uamuzi wa kujenga bomba hilo kupitia Tanzania unatokana na tishio la usalama linalokabili eneo la mpaka wa Kenya na Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako