• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanakijiji wanufaika na mkakati wa kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti na hatua mwafaka

    (GMT+08:00) 2016-04-28 15:37:58


    Kijiji cha Chengzi kiko tarafa ya Mawu, mkoani Gansu nchini China, ni kijiji chenye mandhari nzuri na maliasili nyingi. Lakini kwa sababu kijiji hicho kinazungukwa na milima, hali ya mawasiliano ya barabara ilikuwa nyuma sana, hivyo kwa muda mrefu, umaskini ulikuwa ni tatizo kubwa katika kijiji hicho.

    Kwa miaka kadhaa sasa, China inatekeleza mkakakti wa kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti na hatua mwafaka, na kijiji cha Chengzi vilevile kimenufaika na mkakati huo. Miundombinu ya kijiji hicho imeboreshwa, sura ya kijiji hicho imezidi kuwa nzuri, na wanakijiji pia wamepata njia za kujiongezea kipato, kiwango cha maisha yao kimeongezeka kwa kiasi kikubwa.

    Kijiji cha Chengzi kiko kwenye sehemu ya milima Liupan, ambayo ni sehemu iliyo nyuma zaidi kiuchumi nchini China. Zamani kipato cha wastani cha wakulima wa hapo kilikuwa ni sawa na nusu ya kipato cha wastani cha wakulima nchini China. Lakini kuanzia mwaka 2014 kijiji hicho kilipoanza kutekeleza mkakati wa kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti na hatua mwafaka, hali yake yamebadilika sana. Mkurugenzi wa tarafa ya Mawu Bw. Sun Haifeng anasema,

    "Kabla ya kutekeleza mkakati wa kupunguza umaskini kwa malengo madhututi na hatua mwafaka, kijiji chetu kilikuwa na familia masikini 43 zenye watu 151, ambao wamechukua asilimia 48.5 kati ya watu wote kijijini. Tulikusanya yuan milioni 15 na kuzitumia katika ujenzi wa miundombinu, ukuzaji wa shughuli za kupunguza umaskini na kuboresha huduma za jamii, ili kuwaongoza wanakijiji kupunguza umaskini na kuongeza kipato. Baada ya juhudi za miaka miwili, hivi sasa kijiji chetu kina familia maskini 7 zenye watu 14, ambao wamechukua asilimia 4.5 kati ya watu wote kijijini. Na kipato cha wastani cha wakulima wa kijiji chetu kimefikia yuan 6,800, tumetimiza kimsingi lengo la kupunguza umaskini katika kijiji chetu."

    Katika mchakato wa kutekeleza mkakati wa kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti na hatua mwafaka kijijini hapo, hatua kubwa ya kwanza ni kuboresha mazingira ya maisha na usafiri wa wanakijiji. Zamani kama wakitaka kwenda nje walilazimika kupanda milima kwa miguu, lakini mwaka 2014 barabara yenye umbali wa kilomita 15.4 kati ya kijiji cha Chengzi na tarafa ya Mawu ilijengwa, na wanakijiji wameweza kutumia maji ya bomba na umeme wa nguvu ya jua. Wakati huo huo, miradi ya kuwanufaisha wanakijiji kwa mfano kuwahamishia kwenye nyumba mpya, kuboresha nyumba zenye hatari na kujenga uwanja wa utamaduni, imeboresha sana sura ya kijiji hicho.

    Hivi sasa nyumba mpya za wanakijiji, barabara safi, taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua, zote zimeshuhudia mabadiliko ya kijiji cha Chengzi. Kama ukiingia kwenye nyumba za mwanakijiji, utaona mashine ya maji ya moto inayotumia nishati ya jua, maji ya bomba, vyombo vipya vya matumizi ya kila siku. Mkurugenzi wa kijiji cha Chengzi Bw. Wu Zhiguo alieleza hali tofauti kati ya awali na baada ya kutekeleza mkakati wa kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti na hatua mwafaka. Anasema,

    "Zamani wakulima waliishi maisha magumu, usafiri pia ulikuwa mgumu, barabara haikuwepo, wakati wa mvua tulilazimika kuvaa mabuti, haikuwa rahisi kununua vitu, na ilikuwa ngumu kuuza mazao na mboga, ambayo hayakuweza kusafirishwa na malori. Lakini kwa kupitia kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti na hatua mwafaka, barabara imejengwa, baadhi ya wanakijiji walilia kwa furaha wakati walipoona nyumba zao mpya, ambao awali hawakuwahi kuona nyumba nzuri kama hizo. Kweli nzuri sana."

    Wakati kijiji cha Chengzi kilipohimiza ujenzi wa miundombinu, kilizingatia sana kuwasaidia wanakijiji kupunguza umaskini kutokana na hali halisi ya huko. Kwa mfano, kinahimiza wanakijiji kutumia vizuri maliasili ya kijiji hicho, na kuendeleza shughuli za ufugaji, kupanda miti na utalii.

    Mwaka 2014 Bw. Qin Haijun alirudi kijijini Chengzi na kuanzisha eneo la kufuga kuku, ambao watuuzwa kwenye mikahawa mijini na wageni wanaotalii kijijini. Bw. Qin amesema, hivi sasa sera ya kupunguza umaskini ni nzuri sana, baada ya kufanya kazi mjini kwa miaka sita, anadhani kuwa ni rahisi zaidi kuongeza kipato kwa kupitia ufugaji kijijini kuliko kufanya kazi mijini, pia anaweza kuwaongoza wanakijiji wengine kujiongezea kipato. Anasema,

    "Mwaka 2014 nilirudi nyumbani, kutokana na uungaji mkono wa serikali katika hatua za kupunguza umaskini, nilipanda miti kwa eneo la hekta 2. Mwaka huohuo nilijenga nyumba mpya, mwaka 2015 nilianzisha shirikisho la kufuga kuku 2,000, na kupata faida yuan elfu 40. Kila mwaka kuanzia mwaka huu nitaongeza idadi ya kuku hadi elfu 10. Mimi pia nitapanda majani ya malisho ya mifugo, mwaka kesho nitaanzisha shirika la kufuga ng'ombe, napanga kufuga ng'ombe 50 hadi 100. Mwaka huu nitatoa ombi la mkopo wa yuan laki 5 hadi milioni moja. Shughuli zangu za kufuga kuku na ng'ombe zinahitaji watu, watu wa familia maskini za hapa, wanawake waliobaki kijijini na watu waliokosa ajira mijini, wote naweza kuwaajiri, na kila mtu anaweza kupata yuan elfu 20 kwa mwaka."

    Kama Bw. Qin Haijun alivyosema, ili kuwaunga mkono wanakijiji kukuza shughuli, serikali na benki za huko zimetoa sera nafuu za mikopo. Kijiji cha Chengzi kilianzisha shirikisho la kusaidiana la kupunguza umaskini, ambalo limepewa fedha taslimu yuan laki 4.5 kutoka serikali, linaweza kuipa kila familia inayofanya shughuli za kupunguza umasikini yuan 5000 hadi 10000, hivi sasa shirikisho hilo limetoa mikopo ya yuan laki 2.85 bila riba kwa wanakijiji.

    Mkurugenzi wa tarafa ya Mawu Bw. Sun Haifeng amesema, kijiji cha Chengzi kitakuza sekta ya utalii, ili wanakijiji wapate faida halisi kutokana na mandhari nzuri. Anasema,

    "Kwa upande wa utalii, mandhari ya kijiji chetu iko kwenye bonde la Shiwan na mlima Dayinshan, wakati wa kawaida watalii wengi huendesha magari yao kuja hapa. Baadaye tutapanga kutoa huduma ili kuwasaidia wanakijiji kuongeza kipato. Tunaweza kuandaa vyakula maalum vya kienyeji kwa watalii, pia tunaweza kutoa huduma za kuwaongoza watalii, vilevile tunaweza kuuza bidhaa aina mbalimbali zenye umaalumu wa kienyeji."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako