• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajitahidi kuhimiza maendeleo endelevu ya sekta ya roboti

    (GMT+08:00) 2016-04-27 16:39:10

    Hivi karibuni wizara ya viwanda na upashanaji wa habari, kamati ya maendeleo na mageuzi, na wizara ya fedha ya China zilitoa kwa pamoja mpango wa maendeleo ya sekta ya roboti wa kutoka mwaka 2016 hadi 2020. Naibu waziri wa viwanda na upashanaji habari wa China Bw. Xin Guobin amesema, kwa hatua ijayo wizara hiyo itashirikiana na idara husika na kuchukua hatua za pande sita, ili kuhimiza maendeleo endelevu ya sekta ya roboti ya China.

    Roboti si kama tu ni kifaa muhimu kwenye viwanda vya kisasa, na bali pia ni vifaa vinavyoweza kuboresha njia ya maisha ya binadamu. Utafiti na matumizi ya roboti ni alama muhimu inayoonesha kiwango cha nchi fulani katika kufanya uvumbuzi wa kiteknolojia na kuendeleza viwanda vya kisasa. Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya roboti nchini China imedumisha ukuaji wa kasi. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana China ilitengeneza roboti za viwanda 32,996, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 21.7 kuliko mwaka 2014.

    Ingawa sekta ya roboti ya China imepiga hatua kwa haraka kutokana na sera za uchochezi za kitaifa, lakini katibu mkuu wa Shirikisho la sekta ya roboti la China Bw. Qu Daokui amesema, sekta ya roboti ya China bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa teknolojia muhimu, mnyororo wa viwanda ulio nyuma, na udogo wa sekta nzima.

    "Kwanza ni teknolojia muhimu, mfumo wa udhibiti ni kama ubongo wa roboti, hivi sasa kwa upande wa utengenezaji wa roboti za kawaida, China bado iko nyuma ikilinganishwa na nchi zilizoendelea. Nyingine ni vifaa muhimu vya roboti, ikiwemo mota za umeme, hivi sasa kwa kiasi kikubwa China bado inategemea kuagiza kutoka nje, kiasi hiki kinaweza kufikia asilimia 60 hadi 70."

    Mpango wa kuendeleza sekta ya roboti umeweka malengo makuu ya maendeleo katika miaka mitano ijayo, yaani kukamilisha mfumo wa viwanda vya roboti, uwezo wa kufanya uvumbuzi wa kiteknolojia na nguvu ya ushindani wa kimataifa vinaongezeka kidhahiri, ubora na uwezo wa roboti za China vinafikia kiwango cha kimataifa, maendeleo makubwa yanapatikana kwenye utafiti na utengenezaji wa vifaa muhimu vya roboti, ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko.

    Mpango huo pia unasema ifikapo mwaka 2020, idadi ya roboti zinazotengenezwa nchini China itafikia laki moja kwa mwaka, na mapato ya mauzo ya roboti za kutoa huduma yanatarajiwa kuzidi yuan bilioni 30, haswa kwenye sekta za kuwahudumia walemavu na kutoa msaada wa kimatibabu. Aidha, China pia inatakiwa kuandaa na kuendeleza kampuni tatu kubwa za kutengeneza roboti, vifaa muhimu vya roboti vinavyotengenezwa na China vinatarajiwa kuchukua zaidi asilimia 50 ya mahitaji ya soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako