• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yasema uungaji mkono wa nchi nyingi kwa mpango wa ulinzi wa makombora unatishia usalama wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2016-04-28 09:21:52

    Waziri wa ulinzi wa Russia Sergey Shoigu amesema hivi sasa masharti ya matumizi ya nguvu yamepungua, na uungaji mkono wa nchi nyingi kwa mpango wa ulinzi wa makombora unavuruga utaratibu wa usalama wa kimataifa.

    Bw Shoigu amesema Marekani na NATO wameanza kuimarisha uwepo wao wa kijeshi katika maeneo yaliyo karibu na mipaka ya Russia, kutekeleza mpango wa kinga dhidi ya makombora na kuongeza matumizi ya kijeshi, hatua hizo zote zinailazimisha Russia kuchukua hatua za kijeshi zinazolingana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako