• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Marekani lasema jeshi la nchi hiyo limetia chumvi tishio la China kwenye bahari ya kusini

    (GMT+08:00) 2016-04-28 19:20:07

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, kuna gazeti moja la Marekani linaloona kwamba jeshi la Marekani limetia chumvi tishio la China kwenye bahari ya kusini ya nchi hiyo.

    Bi. Hua Chunying amesema hayo leo baada ya gazeti la Marekani la National Interest kutoa makala inayosema, wasiwasi wa Marekani unaodai kwamba vitendo vya China vya kutetea mamlaka yake kwenye bahari ya kusini ya China vitaathiri biashara ya kimataifa kwenye kanda hiyo, hauna msingi wowote, na pia vitendo hivyo vya China kwenye eneo hilo havitishii usalama wa Marekani.

    Bi. Hua amesisitiza kuwa, China siku zote inaheshimu na kuunga mkono uhuru wa kusafiri kwa mujibu wa sheria za kimataifa, lakini inapinga kithabiti vitendo vyovyote vinavyoharibu mamlaka ya China na maslahi yake ya kiusalama kwa kisingizio cha uhuru wa kusafiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako