• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya madini ya Base Titanium nchini Kenya yatoa ufadhili wa masomo

    (GMT+08:00) 2016-04-28 20:36:03

    Kampuni ya kuchimba madini ya Base Titanium Mining Company imesema itatumia shilingi milioni 15.5 kwenye mpango wake wa kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 350 kutoka familia maskini katika eneo la pwani ya Kenya ambako madini ya Titanium yanapatikana. Wasimamizi wa kampuni hiyo wamesema hatua hiyo inalenga kuwainua wenyeji kimaisha kutokana na ushirikiano mwema ambao wameonyesha kwenye mradi huo. Kampuni hiyo imeongeza kuwa baadhi ya wanafunzi ni werevu ilhali kutokana na umaskini wameshindwa kuendelea na masomo yao ambayo yanaweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadae. Wakati huo huo, waziri wa madini nchini Kenya Bw Dan Kazungu amesema kuna haja ya kutambua utajiri wa madini uliopo nchini Kenya. Amesema kuwa kwa miongo mingi kenya bado haijatambua thamani ya madini yake ilhali yanakadiriwa kuwa ya matrilioni ya pesa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako