• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaweka mkazo katika kupunguza hatari za maafa na kujenga miji salama

    (GMT+08:00) 2016-05-12 17:02:27

    Leo ni maadhimisho ya nane ya kupunguza athari za maafa nchini China, yenye kaulimbiu "kupunguza hatari za maafa na kujenga miji salama". Kutokana na kuharakishwa kwa mchakato wa uendelezaji wa miji, watu wengi zaidi wanahamia mijini na mazingira ya kuishi yameanza kubadilika, wakati huohuo, maafa mbalimbali ya kimaumbile ikiwemo mafuriko, joto kali, radi na matetemko ya ardhi, pia yanatishia usalama wa umma. Leo hii, mazoezi ya kupunguza athari za maafa yamefanyika sehemu mbalimbali nchini China, ili kutoa elimu kwa umma kuhusu ujuzi na ustadi wa kupunguza athari hizo.

    Tarehe 12 Mei mwaka 2008, tetemeko kubwa la ardhi lenye nguvu ya nane kwenye kipimo cha Richter lilitokea huko Wenchuan mkoani Sichuan. Kuanzia mwaka 2009, China ilitangaza kuwa tarehe 12 Mei kila mwaka ni siku ya kitaifa ya kupunguza maafa.

    Mjumbe wa kamati ya wataalamu wa kupunguza athari za maafa ya China Cheng Xiaotao amesema, watu wanapaswa kuwa na ufahamu juu ya hatari za mazingira wanayoishi, kwa mfano, kama maafa ya kimaumbile yanatokea mara kwa mara, na kama yanaweza kuwaathiri. Aidha, hatari pia zinakuwepo kwenye maisha ya kila siku.

    Idara husika zinakadiria kuwa, katika miaka mitano ijayo, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, hali mbaya za hewa itaongezeka kidhahiri, na uwezekeno wa maafa mbalimbali ya kimaumbile kutokea ghafla pia umeongezeka.

    Kutokana na hali hiyo, China imeongeza matumizi ya teknolojia mpya za kisasa kama vile setilaiti na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kupunguza athari za maafa. Huduma ya setilaiti ya usimamizi wa maafa imefunika mikoa 20 nchini China. Ujenzi wa utaratibu wa tathmini ya haraka ya maafa umemalizika kwa hatua ya mwanzo, ambao unaweza kumaliza tathmini ya tetemeko la ardhi saa moja baada ya kutokea na kumaliza tathmini ya dhoruba na mafuriko ndani ya saa tatu.

    Wizara ya mambo ya kiraia ya China imesema, hivi sasa China imejenga kituo cha kitaifa cha kutoa tahadhari za maafa, lakini namna ya kutoa habari za tahadhari haraka iwezekanavyo kwa watu wanaoweza kuathiriwa na maafa, ni suala linalotakiwa kutatuliwa katika miaka mitano ijayo. Naibu waziri wa mambo ya kiraia wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati ya kupunguza athari za maafa ya China Dou Yupei amesema,

    "China inatafiti uwezekano wa kuwa na jukwaa la huduma za uratibu linaloweza kushirikisha mashirika ya kijamii kwenye kazi ya uokoaji wakati wa maafa, pia inajitahidi kukamilisha hatua za kisera zinazohusu mashirika ya kijamii kushiriki kwenye ukoaji wa dharura, matibabu, kuingilia kati kisaikolojia na kueneza ujuzi wa maafa, ili kuziongoza nguvu za kijamii kushiriki kwa utaratibu kwenye kazi mbalimbali za kuzuia maafa, kupunguza athari za maafa na kuokoa maafa."

    Wizara hiyo pia imesema, kutokana na kuendelea kupanuliwa kwa miji na kuongezeka kwa idadi ya watu mijini, China itaharakisha ujenzi wa maeneo ya hifadhi ya dharura wakati wa maafa mijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako