• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pembeni wa Baraza Kuu la Afya Duniani kuhusu visaidizi vya walemavu wafanyika Geneva

    (GMT+08:00) 2016-05-25 14:56:54

    Mkutano mkuu wa afya duniani unafanyika mjini Geneva, ambapo nchi 8 ikiwemo China jana zilifanya mkutano wa pembeni kuhusu visaidizi vya walemavu kwa ajili ya kuboresha teknolojia na kupatikana kwa visaidizi vya walemavu, na kuhimiza ushirikiano katika utoaji huduma kwa walemavu.

    Mkutano huo wa pembeni ulioandaliwa na China, Pakistan, Ujerumani, Ecuador, Korea Kusini, Jamhuri ya Ireland, Marekani na Zimbabwe unahudhuriwa na wajumbe wapatao 100 kutoka nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani WHO, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

    "Visaidizi" ni vitu vinavyosaidia kimaisha walemavu na wazee kama vile vya magurudumu, miguu bandia na vifaa vya kuongeza usikivu. Akihutubia mkutano huo, mkurugenzi wa WHO anayeshughulia dawa muhimu na bidhaa za afya Bibi Suzanne Hill, amesema hivi sasa watu bilioni 1 duniani wanahitaji teknolojia saidizi, lakini ni asilimia 10 tu wanaweza kupata teknolojia hiyo, na inatarajiwa kuwa mkutano huo unaweza kuhimiza kazi katika sekta hiyo. Anasema,

    "Visaidizi ni njia muhimu ya kuzuia ongezeko la gharama za matibabu, na visaidizi vinaweza kuongeza uwezo wa kuhama wa watumiaji, kuhakikisha ubora wa maisha na kupunguza tegemezi kwa huduma za matibabu. Aidha, kazi hiyo inalingana na lengo la usawa linalosisitizwa kwenye ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, na kusaidia watu waliosahauliwa na jamii kuboresha maisha yao."

    Naibu mwenyekiti wa Shirikisho la Walemavu la China Jia Yong ametoa hotuba akisema China imejenga mtandao wa utoaji huduma na visaidizi kote nchini.

    "Kuwahudumia watu wenye ulemavu ni moja kati ya masuala muhimu ya kutekelezwa katika mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano wa China unaoanza mwaka 2016 hadi mwaka 2020. Tunalinda usawa na haki za walemavu, kuboresha maisha yao na kutilia maanani utoaji huduma za visaidizi kwao. Mwaka jana, tulifanya utafiti kwa walemavu milioni 26 waliosajiriwa ili kujua mahitaji yao kwa visaidizi na kuweka msingi wa kutoa huduma zinazowalenga kwa usahihi."

    Bw. Jia amesema kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya utoaji huduma na kusukuma mbele maendeleo ya walemavu yamekuwa maoni ya pamoja ya nchi mbalimbali duniani.

    "Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Kuelekea Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa iliyopitishwa mwaka jana ilijumuisha kwa mara ya kwanza suala la maendeleo ya walemavu, hii imetoa fursa nzuri katika kuendeleza kazi zinazowahusu walemavu. Shirikisho la Walemavu la China linapenda kushirikiana na mashirika ya kimataifa na nchi mbalimbali ili kuchangia maendeleo ya shughuli za walemavu."

    Wakati huohuo, Bw. Jia ametoa wito wa kuunga mkono "Mpango wa Ushirikiano wa Teknolojia Saidizi Duniani" wa Shirika la Afya Duniani WHO, kujenga utaratibu wa vigezo ulio sawa katika sehemu mbalimbali duniani, na pia kuhimiza utafiti wa kisayansi na ubunifu wa huduma wa visaidizi vya walemavu ambavyo watu wanaweza kumudu, viwe rafiki na mazingira na vya teknolojia ya kisasa. Pia amesema nchi mbalimbali zinapaswa kuanzisha utaratibu wa kudumu wa ushirikiano na jukwaa la mawasiliano katika sekta ya visaidizi vya walemavu, na kuongeza nguvu ya uungaji mkono wa kisera nchini humo kwa sekta ya visaidizi na huduma.

    Wajumbe wa nchi nyingine waandaaji pia wamesema kuwapa visaidizi watu wenye mahitaji kama vile walemavu na wazee, kunaweza kuboresha maisha yao na kuwasaidia kujiunga vizuri na jamii. Pia wametoa mwito kwa WHO kutoa "orodha ya visaidizi muhimu" ili kutoa mwongozo kwa nchi mbalimbali katika kuhimiza kazi zinahusiana na utoaji wa visaidizi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako