• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa wanawake wa kundi la nchi 20 wafanyika huko Xi'an, China

    (GMT+08:00) 2016-05-25 16:41:51

    Mkutano wa wanawake wa kundi la nchi 20 ulioandaliwa na shirikisho la wanawake la China umefanyika mjini Xi'an, China na kuhudhuriwa na makamu wa rasi wa China Bw. Li Yuanchao.

    Mkutano huo wenye kaulimbiu "Ushiriki wa Usawa, Ubunifu na Maendeleo" ni sehemu ya mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20, na umeshirikisha wajumbe 200 kutoka nchi wanachama wa kundi hilo, nchi zilizoalikwa, na mashirika ya kimataifa.

    Bw. Li amesema, pendekezo lililotolewa na rais Xi Jinping wa China katika mkutano wa kilele wa wanawake wa dunia limejumuisha makubaliano ya dunia kuhusu ushiriki wa usawa wa wanawake na maendeleo kwa pande zote. Anatarajia kuwa nchi mbalimbali zitafanya juhudi kwa pamoja, ili kutimiza pendekezo hilo.

    Bw. Li pia amesema, China itatekeleza kwa pande zote sera ya msingi ya taifa ya usawa kati ya wanaume na wanawake, na itashirikiana na nchi mbalimbali kutimiza kwa pande zote malengo ya maendeleo ya wanawake ya ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako