• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa ubinadamu wamalizika

    (GMT+08:00) 2016-05-25 16:42:13

    Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa ubinadamu uliofanyika mjini Istanbul, Uturuki, umemalizika kwa kutoa ahadi 1,500.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali za nchi mbalimbali, wafadhili na wenzi wa maendeleo kutekeleza ahadi zao, ili kutimiza "ajenda ya binadamu" yenye majukumu makuu matano haraka iwezekanavyo.

    Bw. Ban pia amesema, Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya juhudi kutimiza malengo ya kazi za kibinadamu, na kuhimiza nchi wanachama kuonesha ushawishi wao na kuunga mkono juhudi husika za Umoja huo. Septemba 19, Umoja huo utaitisha mkutano wa ngazi ya juu kuhusu suala la wakimbizi katika makao makuu yake huko New York.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako