Timu ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys imemaliza katika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya vijana iliyofanyika Goa nchini India.
Serengeti boys walishinda mchezo Wa mwisho dhidi ya Malaysia kwa 3-0 mabao ya vijana wa timu hiyo yalifungwa na Rashid Abdallah, , Shabani Zuberi, na Muhsini Malima, AIFF Youth Cup ni Mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la India, All India Football Federation mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya Mashindano ya yanayowakabili. Michuano hii imetumika kuwapa vijana na timu ya Serengeti mazoezi kujianda na mchezo wao wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Shelisheli .
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |