• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabaki ya siafu wenye sura ya ajabu yagunduliwa

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:04:09

    Siafu walitokea duniani tangu zama za Cretaceous (miaka milioni 145 iliyopita hadi miaka milioni 65 iliyopita), na ni wadudu wenye idadi kubwa zaidi duniani, pia ni wadudu wa kijamii wenye uwezo mkubwa. Lakini kutokana na ukosefu wa mabaki ya kihistoria, watu wanajua habari chache tu kuhusu sura yao ya mwanzoni na mabadiliko yao.

    Baada ya kutafiti sampuli zaidi ya 2000 za mabaki ya siafu yaliyohifadhiwa ndani ya kaharabu, kikundi kinachoongozwa na Dr. Wang Bo kutoka taasisi ya jiolojia na viumbe vya kale ya Nanjing, China kimegundua siafu mwenye sura ya ajabu. Siafu huyu ni wa aina maalum ya siafu wa Haidomyrmex. Ana meno mawili yenye umbo la mundu, ambayo urefu wake ni mara mbili ya kichwa chake. Katikati ya mdomo wake kuna pembe yenye manyoya. Manyoya hayo yanapohisi chakula, siafu huyu anachukua chakula mara moja kwa meno yake mawili na pembe hiyo kama mtego wa panya unavyofanya kazi. Hii ni mara ya kwanza kwa siafu mwenye sura hii ya ajabu kugunduliwa. Dr. Wang Bo alisema siafu walibadilika kuwa aina mbalimbali tangu zama za kale, na mabadiliko hayo ni makubwa kuliko watu walivyofikiria zamani. Tofauti na siafu wa siku hizi ambao ni wadudu wa kijamii, siafu aina ya Haidomyrmex waliishi peke yao. Dr. Wang alisema, "Tukitaja siafu, tunakumbuka hali yao ya kufanya kazi kwa pamoja, lakini utafiti huo unaonesha ukweli kwamba siafu walitumia muda mrefu sana kuelewa kuwa "umoja ni nguvu".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako