• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chaguo gumu zaidi kwa dume--ni kuwavutia jike au kuwa na maisha marefu?

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:06:30

    Utafiti unaonesha kuwa kondoo dume aina ya Soay wenye pembe kubwa wanawavutia zaidi jike, lakini wana maisha mafupi zaidi. Jambo hili linaweza kueleza kwa nini jeni zinazosaidia zaidi kuzaliana hazijarithiwa na viumbe vyote.

    Mwanasayansi aliyetoa nadharia ya mabadiliko ya spishi Charles Darwin alipotafiti manyoya ya rangi mbalimbali ya tausi, aliona uzazi ni sababu muhimu ya mabadiliko ya spishi. Kuwashinda washindani wengine na kuwavutia jike kumewahimiza dume kuwa wakubwa zaidi, kuwa na nguvu zaidi na sura nzuri zaidi. Mchakato huo unaitwa uteuzi kupitia jinsia, unaweza kuathiri jeni za viumbe kama uteuzi asilia ambao unamaanisha viumbe wanaolingana vizuri zaidi na mazingira wanaweza kuishi na kuzaa. Kwa mujibu wa nadharia hiyo, wale wenye nguvu kubwa na sura nzuri tu ndio wanaweza kunusurika katika mazingira ya asili. Lakini hali halisi ni tofauti, dume wadogo na dhaifu pia wamenusurika.

    Mwanabiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh Dr. Susan Johnston na wenzake wametafiti data za kondoo aina ya Soay 1750 wanaoishi katika kisiwa kimoja huko Scottland. Wakarikodi maisha ya kila kondoo na watoto wao tangu mwaka 1985. Wamegundua kuwa kuna aina mbili za kondoo, wale wenye pembe kubwa na wenye pembe ndogo. Kwa wastani kondoo wenye pembe kubwa wanazaa watoto watatu kila mwaka, na wale wenye pembe ndogo wanazaa 1.6 tu. Lakini kiasi cha vifo vya wale wenye pembe ndogo ni asilimia 25 kwa mwaka, na wale wenye pembe kubwa ni asilimia 39. Dr. Johnston anaona kuwa kondoo dume wenye pembe dogo hawana fursa nyingi za kuwa na majike, lakini wana muda mrefu zaidi wa kula na kujitunza.

    Dr. Johnston alisema, kuwepo kwa jeni mbalimbali ni muhimu sana. Kwa mfano, watu wengi wanarithi ugonjwa wa seli mundu(Sickle-cell disease) barani Afrika, lakini wana kinga dhidi ya malaria. Mazao ya kilimo yenye jeni mbalimbali yanasaidia kukinga wadudu. Na kwa viumbe wanaokabiliwa na mabadiliko ya hewa, jeni za aina mbalimbali huenda zikawasaidia kunusurika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako