• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Japani yatoa huduma ya kutabiri hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi kupitia mtandao wa internet

  (GMT+08:00) 2016-06-03 15:45:04

  Taasisi ya utafiti wa saratani ya Japani hivi karibuni imetoa huduma ya kutabiri hatari ya ugonjwa wa moyo na wa kiharusi kwa watu wazima na wazee kupitia mtandao wa internet. Kama ukiweka kiwango chako cha shinikizo la damu na lehemu kwenye tovuti, mtandao huo utakuonyesha hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na wa kiharusi.

  Huduma hiyo inatengemea teknolojia ya mahesabu ya takwimu za kiafya. Kikundi cha watafiti cha taasisi hiyo kimefuatilia watu elfu 15 wenye umri wa miaka 40 hadi 69 katika miaka 16 iliyopita, ambao mwanzoni wote hawakuwa na ugonjwa wa mishipa ya damu au ugonjwa wa moyo.

  Kikundi hicho kilirekodi takimu za afya na tabia za maisha na kujenga mfano wa kutabiri hatari ya ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa kiharusi. Hivi sasa, watu wenye umri wa miaka 40 hadi 69 wanaweza kuweka takwimu zao za kiafya kwenye tovuti na kupata utabiri kuhusu hatari ya kupata ugonjwa wa moyo au kiharusi katika mika 10 ijayo.

  Watafiti wanaona kuwa utabiri huo unaweza kuwasaidia watu kuchukua hatua mapema iwezekanavyo ili kupunguza hatari za kupata maradhi hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako