• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwendo kasi wa kupanuka kwa ulimwengu ni mkubwa zaidi kuliko ulivyokadiriwa

    (GMT+08:00) 2016-06-06 16:22:50

    Wanajimu wakisaidiwa na darubini ya anga ya juu ya Hubble, wamegundua kuwa mwendo kasi wa kupanuka kwa ulimwengu ni mkubwa zaidi kuliko ulivyokadiriwa kwa asilimia 5 hadi asilimia 9. Ugunduzi huo ukithibitishwa, utamaanisha kuwa nadharia ya general relativity(nadharia ya uhusianifu ya jumla) iliyotolewa na Albert Einstein haijakamilika, na msingi wa nadharia za kisasa kuhusu ulimwengu utakabiliwa na changamoto.

    Utafiti huo unaongozwa na mnajimu Adam Guy Riess kutoka taasisi ya sayansi ya uchunguzi wa anga ya juu ya Marekani na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ambaye aliwahi kupata tuzo ya Nobel ya fizikia mwaka 2011 kutokana na kugundua upanuzi wa kasi wa ulimwengu.

    Dk. Riess na wenzake wamehesabu safari za nyota 2400 aina ya Cepheid na nyota 300 aina ya supernova Ia, na kugundua kuwa kila baada ya sekunde milioni moja, umbali kati ya nyota fulani na dunia unaongezeka kwa kilomita 73.2. Hii inamaanisha kwamba katika miaka bilioni 9.8 ijayo, umbali kati ya nyota mbalimbali utapanuka kwa mara moja.

    Lakini tokeo hili haliendani na matokeo ya utafiti mwingine. Umbali uliotolewa na satilaiti ya WMAP iliyorushwa na Shirika la Anga za Juu la Marekani NASA na satilaiti ya Planck iliyorushwa na Shirika la anga za juu la Ulaya ESA ni mdogo kuliko mwendo kasi huo kwa asilimia 5 na asilimia 9.

    Watafiti wamesema tofauti hizi huenda zinatokana na sababu tatu. Kwanza, nishati giza (dark energy) inaitenga mifumo ya nyota kwa nguvu kubwa zaidi kuliko tunavyojua. Pili, mionzi giza (dark radiation) inahimiza ulimwengu kupanuka. Tatu, jambo giza (dark matter) lina uwezo wa ajabu. Ugunduzi huo mpya utawahimiza wanasayansi kufikiria tena ulimwengu, hasa mawazo kuhusu jambo na nishati giza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako