• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwanini mafuriko hutokea katika nchi mbalimbali?

    (GMT+08:00) 2016-06-08 13:33:28

    Nchi mbalimbali duniani zinakabiliwa na mafuriko. Sehemu za kusini mwa China zinakabiliwa na mvua kubwa, wataalamu wametoa onyo kwamba mafuriko makubwa huenda yatatokea. Ufaransa na Australia pia zinakabiliwa na mvua kubwa inayoendelea kwa siku nyingi. Je, hali ya hewa mbaya katika nchi hizi zina sababu zinazolingana?

    Idara ya hali ya hewa ya China imesema shinikizo kubwa la hewa katika ukanda wa subtropic ulioko magharibi mwa bahari ya Pasifiki huleta mvua nchini China katika majira ya joto. Lakini mvua za El Nino zinavuruga hali ya kawaida, kupanua eneo lenye shinikizo kubwa la hewa, kuongeza shinikizo hilo, kusababisha mvuke mwingi zaidi kuingia katika nchi kavu na kuleta mvua nyingi zaidi nchini China.

    Tukio la La Nina hutokea baada ya Mvua za El Nino. Kinyume na El Nino, La Nina inamaanisha maji ya bahari ya Pasifiki yanabadilika na kuwa baridi. Tukio hili husababisha mvua kubwa nchini Australia katika majira ya baridi na mpukutiko.

    Mafuriko yaliyotokea nchini Ufaransa yamewalazimisha wakazi zaidi ya elfu 20 kuhama. Waziri wa mazingira ya ikolojia, maendeleo endelevu na nishati Bibi Marie-Segolene Royal alisisitiza kuwa mvua kubwa zitanyesha zaidi kutokana na kuongezeka kwa joto duniani. Ingawa baadhi ya wataalamu wa hali ya hewa walisema ni vigumu kuhusisha hali ya hewa mbaya na kuongezeka kwa joto duniani, lakini watu wengi wamekubali kwamba hali ya hewa mbaya hutokea mara nyingi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako