• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aina mbili za chatu wamepata hulka zinazofanana kutokana na mazingira yanayofanana

    (GMT+08:00) 2016-06-16 15:09:41

    Python na boa wote ni chatu wakubwa, urefu wa Python Reticulatus na boa aina ya Eunectes Murinus wote unaweza kufikia mita 8, na wote wanaua mawindo kwa kuwashika kwa miili yao. Lakini ukweli ni kwamba python na boa ni tofauti, python wanataga mayai, na boa wengi wanazaa chatu wachanga moja kwa moja.

    Baada ya kutafiti vichwa vya sampuli 2000 za python na boa zilizokusanywa kutoka bara la Amerika na Australia, watafiti wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia waligundua kuwa ingawa chatu hao wamebadilika katika historia ndefu, lakini kutokana na mazingira yanayofanana, wamepata sura na hulka zinazofanana. Python na boa wanaoishi majini, mapangoni au misituni wote wana sura zinazofanana.

    Hali hii inaitwa mabadiliko yanayokutanisha (convergent evolution), ambayo yanamaanisha kuwa spishi tofauti zinapata hulka zinazofanana ili kuendana na mazingira yanayofanana.

    Mtafiti Damien Esquerre alisema mabadiliko hayo yameonesha athari kubwa ya chaguo la maumbile, na uwezo wa viumbe wa kuendana na mazingira.

    Katika mazingira ya viumbe, kuna mifano mingi inayoonesha mabadiliko yanayokutanisha. Kwa mfano, maumbo ya miili ya papa ambaye ni samaki na pombe ambaye ni mamalia yanafanana. Na chui milia wa Tasmanian mwenye pochi ya kuwalea wachanga ambaye ametoweka duniani anafanana na mbwa mwitu ambaye hana pochi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako