• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Licha ya mwezi, dunia yetu imepata mwezi mwingine

    (GMT+08:00) 2016-06-20 09:54:44

    Wanajimu wamegundua sayari ndogo inayozunguka dunia yetu wakati inapozunguka jua, na kuipa jina la "2016 HO3". Iko mbali na dunia yetu, hivyo hatuwezi kuichukulia kuwa ni satilaiti kama mwezi, lakini imeizunguka dunia kwa muda mrefu, inaweza kuchukuliwa kuwa ni "nusu satilaiti".

    Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa magimba ya angani yaliyoko karibu na dunia cha maabara ya JPL ya Shirika la safari za anga ya juu la Marekani NASA Bw. Paul Chodas alisema, satilaiti nyingine ndogo iitwayo "2003 YN107" iliwahi kuizunguka dunia katika zaidi ya muongo mmoja uliopita, lakini imeondoka. Sayari ya "2016 HO3" itaizunguka dunia kwa muda mrefu zaidi, imeizunguka dunia katika karne moja iliyopita, na itaendelea kufanya hivyo katika karne kadhaa zijazo.

    Kila mwaka sayari hiyo inalizunguka jua kwa mzunguko mmoja kama dunia inavyofanya. Katika nusu mwaka ya kwanza inakuwa karibu zaidi na jua kuliko dunia, na katika nusu nyingine inakuwa mbali zaidi na jua kuliko dunia. Kwa sababu inaposafiri mbele au nyuma kupita kiasi, mvutano wa dunia inairudisha, na inaonekana kama inacheza dansi na dunia.

    Sayari hiyo iligunduliwa tarehe 27 Aprili mwaka huu na darubini ya anga ya juu ya Pan-STARRS 1 iliyoko huko Hawaii. Ukubwa wa sayari hiyo bado haujapimwa, lakini inakadiriwa kuwa ni kati ya mita 40 hadi 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako