• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Njia mpya ya kupunguza uzito--kuamsha mafuta kahawia ndani ya mwili wako

  (GMT+08:00) 2016-06-20 15:47:48

  Mafuta meupe ndani ya miili ya binadamu yanatumiwa kuhifadhi nishati, na mafuta ya kahawia yanatumiwa kuzalisha joto. Kwa watu wanene, kuyafanya mafuta ya kahawia yazalishe joto jingi zaidi kunasaidia kupunguza uzito. Watafiti wa Chuo Kikuu cha Leipzig cha Ujerumani wamegundua njia mpya ya kupunguza uzito kupitia kupunguza mafuta kahawia.

  Katika miaka mingi iliyopita, wanasayansi waliona mafuta ya kahawia yanafanya kazi nyingi zaidi katika miili ya watoto. Lakini utafiti uliofanyika katika miaka ya hivi karibuni unaonesha kuwa mafuta ya kahawia ndani ya miili ya watu wazima pia yanaweza kuamshwa, na baadhi ya mafuta meupe yanaweza kubadilishwa kuwa kahawia.

  Watafiti walipofanya majaribio kwa kutumia panya, wamegundua kuwa kemikali iitwayo Phosphodiesterase 10A ndani ya mafuta ya mwilini. Kazi ya kemikali hiyo ikizuiliwa, mafuta ya kahawia yataamshwa, baadhi ya mafuta meupe yanabadilika kuwa kahawia, uzito wa panya utapungua kwa kiasi kikubwa, na uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari utapungua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako