Wapalestina wanne waliowaua wanandoa wa Israel katika mashambulizi ya sehemu ya magharibi mwa Mto Jordan mwaka jana wamehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya kijeshi ya Israel.
Mahakama ya kijeshi ya Smaria ya ukingo wa magharibi mwa Mto Jordan pia imetoa hukumu mbili za kifungo cha maisha na miaka 30 gerezani kwa watu hao.
Wapalestina hao walikutwa na hatia ya kupanga na kufanya mashambulizi mwaka jana kwenye sehemu ya magharibi ya Mto Jordan na kusababisha vifo vya Eitam na Naam Henkin waliofanya matembezi pamoja na watoto wao wanne. Pia wametajwa kuwa ni wanachama wa kundi la Hamas.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |