• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli ataka mamlaka husika kuhakikisha kodi inakusanywa ipasavyo

    (GMT+08:00) 2016-06-23 20:05:28

    Rais John Pombe Magufuli ameagiza taasisi zinazosimamia fedha na kodi, kuhakikisha kuwa serikali inakusanya kodi kwenye miamala ya fedha, inayofanywa na taasisi hizo na kampuni za simu na za madini.

    Magufuli pia ameagiza kuwa Shilingi bilioni saba zilizolipwa kwa pensheni hewa, zirejeshwe mara moja huku akitoa ufafanuzi wa hatua ya serikali ya kusitisha kwa muda ajira serikalini.

    Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), rais Magufuli amesema takwimu zinaonesha katika mwezi wa Machi, miamala iliyofanywa na kampuni za simu za mkononi ni ya zaidi ya Shilingi trilioni 5.5, lakini alihoji ni kasi gani cha kodi kimeingia serikalini. Magufuli ameagiza BoT, Hazina na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wajipange kuhakikisha mtambo wa kudhibiti makusanyo ya kodi, unafanya kazi na kufuatilia usalama wa huduma za fedha. Mbali na hilo, alizitaka tahasisi hizo kuhakikisha serikali inakusanya kodi zinazostahili kutoka kwenye kampuni za madini na kufuatilia kwa karibu, kwa kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya kampuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako