• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:TBA yakusanya bilioni 2.6

    (GMT+08:00) 2016-06-24 17:24:35

    Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umekusanya Sh bilioni 2.6 ikiwa ni zaidi ya asilimia 40 ya madeni waliyokuwa wakiwadai watumishi wa umma na watu binafsi waliouziwa na kupanga nyumba za serikali kwa makazi na biashara.

    , Mkurugenzi Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga amesema kabla ya kulipwa kwa fedha hizo, wakala huo ulikuwa ukidai zaidi ya Sh bilioni sita ambapo baada ya kutolewa kwa notisi ya kulipa tayari wamekusanya Sh bilioni 2.6.

    Mwakalinga alisema shughuli ya kuwatoa wapangaji wengine inaendelea katika mikoa mbalimbali, na mkoani Dodoma wamewaondoa wapangaji katika nyumba 27 huku Mwanza shughuli hiyo ikikwama baada ya kuibuka fujo kati ya mpangaji na mfanyakazi wa Kampuni ya Udalali ya Yono ambao ni wasimamizi katika shughuli hiyo.

    Wwakala huo unataka fedha kuirudi ili waendelee na ujenzi wa nyumba nyingine, kuregesha fedha zilizofujwa .

    Alisema ili kuondoa tatizo la ucheleweshwaji wa ulipaji kodi katika nyumba hizo kuanzia Julai wapangaji binafsi wataanza kulipa kodi kwa miezi sita huku watumishi wa umma wakiendelea kulipa kwa miezi mitatu mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako