• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 42 wa kundi la IS wauawa katika mashambulizi ya anga nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2016-06-25 18:28:31
    Kituo cha televisheni cha Tolo kimeripoti kwamba wapiganaji 42 wa kundi la IS wameuawa na wengine 32 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa leo na ndege zisizo na rubani mkoani Nangarhar, mashariki mwa Afghanistan.

    Habari zinasema, mashambulizi hayo yaliwalenga wapiganaji wa IS walioko maeneo ya Kot na Achin, ambayo yameaminika kuwa ngome ya IS nchini Afghanistan.

    Mpaka sasa kundi la IS halijatoa maoni juu ya mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako