• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yanasa tani 15.6 za dawa za kulevya tangu 2014

    (GMT+08:00) 2016-06-26 18:01:06

    Mamlaka ya forodha nchini China imenasa tani 15.6 za dawa za kulevya zilizoingizwa nchini humo kimagendo tangu mwaka wa 2014.

    Dawa hizo ambazo ni pamoja na heroine, cocaine, methamphetamine na opium, zilinaswa kwenye kesi 1,091 zinazohusisha washukiwa zaidi ya 1,055.

    Nyingi za dawa hizo zilinaswa kwenye ukaguzi wa watalii, vifurushi kwenye posta na makampuni ya kusafirisha bidhaa.

    Njia za magendo ya dawa za kulevya zimeendelea kuwa ngumu kugundulika, kwa mfano mamlaka za forodha mjini Shanghai zilipata dawa zikiwa zimefichwa kwenye mvinyo, na mjini Qingdao dawa zilipatikana zikiwa zimefichwa kwenye nguo za ndani.

    Pia imebainika kwamba walanguzi wa mihadarati wanawatumia kina mama wajawazito, watoto na wazee kubeba dawa za kulevya.

    Habari nyingine zinasema, ndani ya mwaka mmoja uliopita polisi nchini China wamewakamata karibu washukiwa 134, 000 wanaohusika na kesi 113, 000 za uhalifu wa mihadarati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako