• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga wakomeshwa na TP-mazembe 1-0

    (GMT+08:00) 2016-06-29 08:20:55

    Klabu ya Yanga ya Dar es salaam Tanzania imepoteza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika kwa kufungwa bao 1-0 na TP-mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es salaam, Yanga ilionesha kandanda safi katika kipindi cha kwanza, kabla ya TP Mazembe kubadilika katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao hilo lililofungwa dakika ya 74 na kiungo Merveille Bope.

    Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kupoteza ukitanguliwa na ule uliochezwa nchini Algeria Juni 19 na kufungwa bao 1-0 na MO Bejaia.

    Kwa matokeo haya, hadi sasa TP Mazembe inasalia kileleni kwa kuwa na pointi 6, huku Yanga ikiwa haina point hata moja, katika kundi A.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako