• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watafiti wa Australia wapiga hatua katika kuendeleza chanjo dhidi ya ugonjwa wa malaria

  (GMT+08:00) 2016-07-01 19:02:06

  Watafiti wa Australia wamepiga hatua katika kuendeleza chanjo dhidi ya ugonjwa wa malaria.

  Watafiti kutoka taasisi ya Walter and Eliza Hall wamegundua njia ya kuzuia kimelea cha malaria kuvamia chembe nyekundu za damu zenye afya.

  Profesa Alan Cowman aliyeongoza utafiti huo ametoa taarifa akisema, kimelea cha malaria hakiwezi kupenya katika chembe nyekundu za damu za binadamu wakati protini muhimu zikiondolewa.

  Cowman amesema, ugunduzi huo unatarajiwa kusaidia kufahamu uwezo wa protini hizo na kuziendeleza kama chanjo, huku akisema kuendeleza chanjo mpya dhidi ya malaria ni kipaumble cha utafiti wa kimataifa.

  Imefahamika kwamba ugonjwa huo unaua watu hadi laki 4.5 kila mwaka hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako