• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan yapanga kutumia udongo wenye uchafuzi wa nyuklia katika ujenzi wa barabara

    (GMT+08:00) 2016-07-04 14:35:02

    Wizara ya mazingira ya Japan hivi karibuni imepanga kutumia udongo mita milioni 10 za ujazo wenye uchafuzi wa nyuklia unaotoa mionzi chini ya Bq 8000 kwa kilo katika ujenzi wa barabara. Lakini masuala ya kuhakikisha usalama wa udongo huo na usimamizi wa muda mrefu bado hayajatatuliwa, hivyo vyombo vya habari vya Japan vimesema mpango huo huenda ukaongeza wasiwasi wa kuenea kwa uchafuzi wa nyuklia.

    Gazeti la Mainichi la Japan limeripoti kuwa wizara hiyo imepanga kutumia udongo wenye uchafuzi katika ujenzi wa barabara, na kuweka udongo, mchanga na saruji juu ya udongo wenye uchafuzi ili kuzuia mionzi.

    Baadhi ya vyombo vya habari vimesema mionzi chini ya Bq 8000 kwa kilo ni kigezo cha kushughulikia takataka zenye uchafuzi wa nyuklia, na si kigezo cha kuzitumia tena kwa usalama, hivyo uamuzi wa serikali huenda ukaleta wasiwasi kwa watu.

    Suala la kuufanya udongo mwingi wenye uchafuzi kufikia kigezo cha usalama cha Bq 100 kwa kilo bado halijatatuliwa.

    Baada ya ajali kutokea katika kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima, idara husika za Japan zimeondoa udongo mita milioni 22 za ujazo wenye uchafuzi wa nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako