• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo lisilo na hewa ya ozoni katika anga ya ncha ya kusini ya dunia limepungua

    (GMT+08:00) 2016-07-05 14:17:26

    Ripoti iliyotolewa hivi karibuni kwenye gazeti la Sayansi la Marekani inasema eneo lisilo na hewa ya ozoni katika anga ya ncha ya kusini ya dunia limepungua kwa kiasi kikubwa, hali hii inaonesha kuwa juhudi za binadamu za kupinga marufuku utoaji wa hewa ya CFC imepata mafanikio. Prof. Susan Solomon wa Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts amesema kwa mujibu wa data zilizopatikana kupitia satilaiti, vifaa vya uchunguzi wa ardhini na maputo ya uchunguzi, eneo lisilo na hewa ya ozoani katika ncha ya kusini ya dunia mwezi Septemba mwaka jana limepungua kwa kilomita milioni 4 za mraba kuliko lile la mwezi Septemba mwaka 2000, eneo lililopungua ni kubwa zaidi kuliko India.

    Hewa ya Ozoni iliyoko katika anga ya juu inaweza kuvuta mwanga wa Ultraviolet, na kuhifadhi viumbe wa duniani. Lakini hewa ya CFC inayotolewa na binadamu inaharibu hewa ya Ozoni, hivyo mwaka 1987 jumuiya ya kimataifa ilipitisha makubaliano ya Montreal kudhibiti uzalishaji na matumizi ya CFC.

    Mwaka 2011 watafiti waligundua dalili ya kupungua kwa eneo lisilo na hewa ya ozoni, ripoti iliyotolewa na Shirika la hali ya hewa duniani mwaka 2014 pia limeeleza jambo hili, na utafiti mpya umelithibitisha.

    Uchunguzi hufanyika mwezi Septemba wakati kipindi chenye usiku mrefu kinapomalizika huko ncha ya kusini ya dunia. Hewa ya CFC inapoharibu hewa ya Ozoni inahitaji mwanga wa jua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako