Uganda iko katika mchakato wa kukamilisha mpango wa maendeleo ambayo utaiona nchi hiyo ikianzisha maeneo 10 huru ya biashara ifikapo mwaka wa 2020.
Nafasi hizi huru za biashara zitakuwa na uwezo wa kuzalisha dola bilioni 1 kwa mwaka na dola milioni 100 kwa mauzo ya nje.
Aidha, nafasi hizo huru za biashara zitafungua nafasi 2,500.
Jabo anasema motisha hii itaruhusu wawekezaji kuzalisha, kiasi kikubwa na bidhaa bora katika kiasi ushindani wa gharama ya chini kwa soko la nje.
Waziri wa mipango nchini uganda bw: David Bahati amesema uganda kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbili za kiuchumi ambazo ni; ajira kwa vijana na jinsi ya kukabiliana na kilimo cha kujikimu.
Bahati pia amesema lengo la serikali mwaka huu wa fedha ni jinsi ya kujenga na kutoa nafasi za ajira kwa watu wa Uganda kwa kuzingatia asilimia 75 ya vijana Uganda hawana ajira.
Serikali pia inapanga jinsi ya kupata kaya milioni 4.8 kushiriki katika kilimo cha kujikimu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |