• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali Tanzania kujenga shule za michezo kila mkoa

    (GMT+08:00) 2016-07-06 08:41:25

    Serikali ya Tanzania imeazimia kujenga na kuendeleza shule za michezo zilizopo katika mikoa yote kwa kipindi hiki cha Serikali awamu ya tano.

    Azimio hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati akizungumza na timu ya mpira ya miguu ya wasichana ya FC Vito Malaika katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup yatakayofanyika nchini Finland Julai 8.

    Amesema Serikali ya Tanzania inashirikia na Serikali ya Finland katika kuendeleza michezo shuleni na zaidi ya shule 462 nchini zitafaidika na miradi ya michezo ya vijana inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako