• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Afrika yatakiwa kuimarisha sekta ya viwanda

    (GMT+08:00) 2016-07-18 19:36:17

    Afrika inahitaji juhudi za pamoja kukuza sekta ya viwanda ambayo itasaidia kunyanyua uchumi wa bara la Afrika, kupunguza umasikini na kuleta maisha bora.

    Hayo yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa NEPAD, chombo cha utendaji cha Umoja wa Afrika, Dk Ibrahim Mayaki, wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Umoja wa Afrika zilizopo kwenye mpango huo wa maendeleo barani Afrika.

    Kwa upande wa ajira na viwanda, Dk Miyaki alisema bara la Afrika kwa sasa lina vijana wengi kuzidi mabara mengine duniani, hivyo kuna nguvu kazi kubwa ambayo isipotafutiwa mpango mahsusi wa ajira umasikini utazidi barani humo.

    Alisema, viwanda vya Afrika vikiongezeka, ajira kwa vijana zitapatikana, uzalishaji utaongezeka na biashara ndani ya Afrika itashamiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako