• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makosa unayoweza kufanya wakati unapowapa watu huduma ya kwanza

  (GMT+08:00) 2016-07-20 09:33:08

  Watu wengi sasa wana ujuzi wa huduma ya kwanza, wakikutana na hali ya dharura huwa hawahangaiki kama zamani. Lakini njia zisizo sahihi wanazotumia zinaweza kuharibu miili yao. Yafuatayo ni makosa wanayoweza kufanywa wakati wa huduma ya kwanza:

  1. Kuinua kichwa cha chako wakati pua yako ikitokwa na damu, lakini, kufanya hivyo kunaweza kusababisha damu kutiririka na kuingia kwenye koo na kusababisha ukosefu wa hewa. Na hasa ukitokwa na damu puani baada ya kujeruhiwa, usitumie vitu vyovyote puani kuzuia damu hiyo kutoka, kwani ukifanya hivyo, inawezekana ukasababisha ubongo wako kuambukizwa na virusi.

  2. Watu wengi wakiungua, wanapendelea kutumia dawa ya meno kupunguza maumivu, lakini kufanya hivyo kunaweza kusababisha mahali palipoungua kuambukizwa na virusi kwa hivyo njia sahihi ya kushughulikia ni kutumia maji baridi kusafisha na kupunguza digrii ya joto palipoungua.

  3. Kusaidia wazee walioanguka kusimama mara moja.

  Kwani mifupa ya wazee wengi huvunjika kirahisi, wakianguka na wakavunja mifupa yao mwilini, ukiwasaidia kusimama mara moja basi mzee anaweza kujeruhiwa zaidi. Kwa hivyo, ukikutana na mzee aliyeanguka na ukishuku kwamba amevunjika mifupa yake, bora usimwinue mwache na usubiri gari la wagonjwa, lakini akitokwa na damu, bora umsaidie kuzuia kutoka na damu kwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako