• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini unga mweupe hutokea baada ya maji kuchemka?

    (GMT+08:00) 2016-07-21 10:41:52

    Ukichemsha maji, unga mweupe huonekana majini. Birika likitumiwa kwa muda mrefu, ndani yake litakuwa na utando mgumu mweupe.

    Lakini unga huo unatoka wapi? Kwanza tunahitaji kupata ujuzi kidogo kuhusu maji. Kuna maji magumu na laini. Mvua na theluji ambayo hayana kemikali nyingi za Calsium na Magnesium yanaitwa maji laini. Maji ya maziwani, mitoni, visimani na chemichemi yenye kemikali hizi nyingi yanaitwa maji magumu, na maji ya bomba yaliyozalishwa kwa kusafisha yale ya maziwani na mitoni pia ni magumu. Mwanzoni kemikali mbalimbali zikiwemo Calcium Bicarbonate na Magnesium Bicarbonate zinayeyuka majini, lakini maji yakichemka, kemikali hizi zinavunjika na kuunda kemikali mpya zikiwemo Calcium Carbonate na Magnesium Carbonate ambazo haziwezi kuyeyuka majini. Kemikali hizi zinajichuja chini na kuunga utando mweupe ndani ya birika siku hadi siku.

    Lakini utando mweupe ukionekana ndani ya birika na chupa za maji, unauondoa vipi? Calcium Carbonate na Magnesium Carbonate zote zinaweza kubadilishwa na kemikali za asidi, hivyo ukimimina siki ndani ya birika, na kuichemsha kidogo, utaona vipovu vingi vinatokea juu ya utando huo, halafu utatoweka. Pia unaweza kuondoa utando ndani ya chupa kwa njia hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako