• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baadhi ya siafu wanalima kama binadamu!

    (GMT+08:00) 2016-07-25 07:07:08

    Binadamu wanafanya shughuli za kilimo ili kupata chakula, lakini unajua siafu nao pia wanaweza? Baadhi ya siafu wanalima kuvu ili kupata lishe ya protini, mafuta na carbohydrate.

    Watafiti wamechambua jeni za aina 7 za siafu wanaolima kuvu, na kugundua kuwa siafu walipata uwezo huo miaka milioni 55 hadi milioni 60 iliyopita, lakini wakati huo walilima kuvu wa aina mbalimbali bila kuchagua. Kuanzia miaka milioni 30 iliyopita, aina tofauti za siafu walianza kuchagua kuvu tofauti inayowafaa. Baadaye walibadilika kuwa siafu wenye uwezo mkubwa zaidi, walianza kukata majani kuwa vipande vipande na kupanda kuvu katika masalio ya majani.

    Lakini kwa nini siafu wanalima? Baada ya kutafiti jeni za siafu wanaokata majani, watafiti wamegundua kuwa siafu hao hawana uwezo wa kuzalisha lishe ya Arginine miili mwao. Ukosefu wa Arginine utaathiri maisha yao, hivyo siafu hao wakajaribu kupata lishe hiyo kutoka kwenye kuvu.

    Kiongozi wa kikundi cha utafiti wa jeni za viumbe mbalimbali cha benki ya Jeni ya China Bw. Zhang Guojie alisema siafu hawa ni mfano mzuri unaoonesha viumbe viwili vinabadilika kwa pamoja. Si kama tu siafu wamebadili jeni za kuvu, bali pia jeni zao zimebadilika ili kuendana na maisha ya kilimo, hali hii pia imetokea kwa binadamu tangu waanze kufanya shughuli za kilimo. Hali hizi zinazofanana hazikutokea kwa bahati, zinaonesha kanuni za kimaumbile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako